Tasnia ya michezo ya bahati nasibu inakua kwa Kasi ya ajabu kutokana na kuongezeka kwa watumiaji wengi wa intaneti, na kukua kwa miamala ya kifedha.
Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imezidi kuwa Soko pendwa katika biashara hii inayotajwa kushika nafasi za juu kuwa na mkwanja mrefu.
Je Tanzania inanufaika vipi na kampuni hizi?
1. Kuinuka kwa sekta ya michezo. Kampuni za beti zimekuwa zikiwekeza pakubwa katika kuinua michezo nchini. Mfano vilabu kadhaa hudhaminiwa na kampuni za kubeti Kama ifuatavyo
A, Mbeya City kwa miaka kadhaa klabu ya Mbeya City imekuwa ukidhaminiwa na Kampuni ya Parmatch Tanzania
B. Ujenzi wa viwanja na uboreshaji wake, kazi hii imefanywa pakubwa na kampuni ya Premierbet Tanzania.
C. Simba, kwa miaka kadhaa Simba imekuwa ukidhaminiwa na sportpesa na Sasa M-bet
D. Yanga, kwa miaka zaidi ya 6 yanga imekuwa ukidhaminiwa na sportpesa, sawia na Namungo pamoja na Singida star.
E. KMC kwa sasa klabu Cha KMC kinadhaminiwa na wakongwe wa beti Tanzania Meridian bet,
F. 10bet inayodhamini Dodoma jiji
Haya ni maendeleo makubwa katika kuinua soka letu, tunatarajia vilabu vingine kuendelea kunufaika na kampuni hizi siku za usoni.
2. AJIRA KWA WATANZANIA, kampuni za betting pia zimekuwa zikitoa ajira mbalimbali kwa watanzania pamoja na kutoa fursa mbalimbali za matangazo katika vituo mbalimbali vya redio, MAGAZETI, televisheni, pamoja na mawakala wa matangazo mbalimbali.
3. NI CHANZO CHA MAPATO KWA BAADHI YA WATANZANIA. Baadhi
ya watanzania hasa vijana hutegemea kampuni hizi kujipatia chochote,
4. HUJENGA UCHUMI KWA KULIPA KODI, Serikali imekuwa mstari wa mbele kukusanya MAPATO kutoka katika kampuni hizi ambapo tunaamini kuwa kutokana na mapato hayo tunaweza kupata maendeleo ya kiuchumi. Hata hivyo mwandishi wa makala hii anashauri tuangalie uwezekano wa mapato yanayopatikana katika tasnia ya michezo ya bahati nasibu yatumike kwa kiasi kikubwa kuboresha timu zetu za Taifa.
Mwisho serikali na Wadau wanaohusika waendelee kutengeneza mazingira rafiki ya kampuni zaidi ya michezo ya bahati nasibu kuja kuwekeza tanzania ili tuzidi kunufaika nazo. Mwisho kwa wachezaji wote wa michezo hii wanakumbushwa kucheza kisataarabu.
Source www.masshele.com