Wiki imeanza vyema zaidi kwa Klabu ya soka ya KMC, ambao wamepata mdhamini mpya, ikiwa ni neema kwa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania. KMC wameingia rasmi mkataba wa udhamini na Meridianbet, ambao ni mabingwa na Kampuni ya kwanza ya ubashiri Tanzania.
KMC imekuwa ni klabu inayokua kwa kasi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014, ikiwa haijawahi kushuka daraja tangu ipande ligi kuu. Ni timu inayoonesha uwezo, katika kusalia kwenye ubora wa Ligi kuu Tanzania, moja ya Ligi zenye ushindani mkubwa sana barani Afrika kwa zaidi ya miaka 7.
Msimu ukiwa mbichi kabisa, KMC inajipanga kufanya vyema zaidi msimu huu. Meridianbet, wameamua kuwashika mkono kwenye safari yao kwa mkataba wa miaka mitatu.
Meridianbet wamebainisha kuwa huu ni mwendelezo wa jitihada zao za ‘kusapoti’ michezo duniani, kuinua vipaji na kurejesha kwa Jamii yake (CSR). Kampuni hii imedhamini vilabu zaidi ya 20 duniani. Kwa Tanzania, Meridianbet, ambao wamejikita katika ubashiri wa michezo na kasino mtandaoni, wamefanya udhamini katika ngazi mbali mbali, kuanzia mashinani hadi ligi daraha la kwanza, kwa soka la wanawake na wanaume.
“Huu sio mwanzo kwetu kujihusisha na soka, ni muendelezo wa jitihada tulizokuwa tukizifanya toka ngazi za chini, kwa kutoa sapoti kwa vilabu mbali mbali vinavyochipukia. Tumefanya ligi za wanawake na vijana, tukiwa kama Kampuni bora, tumefurahi kushirikiana na klabu bora” – Chetan Chudasama, Mkurugenzi wa Kampuni ya Meridianbet.
Akizungumza, kwa niaba ya KMC, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Songoro Mnyonge, amesema wamefurahi kupata mdhamini mwingine bora, na kwa kuwa na wao ni klabu bora, wataendelea kushirikiana yema kurejesha thamani ya udhamini huu kwa miaka mitatu ijayo.
“Kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi, kwa kuwa sisi ni bora, ubora wetu umetuletea mdhamini mwingine ambaye ni Meridianbet. Tunamtambulisha kwenu Meridianbet kuwa mdhamini wetu mkuu kwa miaka mitatu.”
Meridianbet wanabainisha kuwa wataendelea kujihusisha zaidi na michezo, na wanatazamia kuona mafanikio makubwa na klabu ya KMC ndani ya miaka ijayo.
“Kama kampuni tunatazamina kuona klabu hii ya KMC inafanikiwa na tutaendelea kuwa bega kwa bega kuhakikisha tunafanikiwa pamoja. Tunajivunia kuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya soka linapokua na kutoa fursa mbali mbali za kiuchumi na kuwaleta watu pamoja.” – Twaha Mohamed, Afisa Masoko wa Meridianbet.