Kampuni kongwe ya michezo ya kubashiri mtandaoni M-bet inayotoa huduma zake Tanzania, Kenya na Uganda, imesaini kandarasi ya miaka 5 kuwa mdhamini mkuu wa klabu ya kandanda ya SIMBA yenye maskani yake mtaa wa msimbazi Dar es salaam.
Bado dili rasmi halijatajwa lakini taarifa za awali zilizotolewa na pande mbli hizo zimedhibitisha kusainiwa kwa kandarasi hiyo huku walisema taarifa zaidi zitakuja jumatatu.
Kwanini M-bet, Awali sportpesa kwa miaka kadhaa ndio umekuwa ikiidhamini Simba, Yanga na Namungo na dili lao na Simba lilifika ukomo mapema mwezi huu.
Huenda Simba ineshindwa kuendelea na udhamini wa Sportpesa kutokana na kushindwana kwa maslahi au mdhamini kutopata faida aliyoilenga ndani ya klabu hiyo yenye wafuasi wengi katika Mtandao wakijamii. Hata hivyo Hilo linabaki Kama kitendawili.
M-bet watafaidika?
Kwa majibu ya namna tasnia ya michezo ya bahati nasibu ilivyo jibu linaweza kuwa ndio. Kutokana na wingi wa mashabiki wa Simba hasa wafuatiliaji katika mitandao ya kijamii.
Soma pia >>Kampuni Bora za kubeti tanzania
Sportpesa anaelekea wapi?
Kutokana na sportpesa kupoteza mdau muhimu katika suala zima la masoko huenda Nguvu zake zote akazielekeza kwa watani wa Simba , Yanga , pamoja na timu nyingine yenye Nguvu ligi kuu kwa msimu ujao Kama vile Singida big staar au kunako Azam FC.
Hata hivyo tutarajie ushindani mkubwa katika miaka ya baadaye hasa katika masuala haya ya udhamini