Dar es Salaam. Valerian Massawe (36) kutoka Kiluvya, Pwani ameandika historia ya kuibuka mshindi wa zawadi ya kitita cha fedha Sh1.2 bilioni kutoka Kampuni ya michezo na burudani ya SportPesa baada ya kutabiri kwa usahihi mechi 13 za Jackpot ya wiki iliyopita ya Kampuni hiyo.
Massawe ambaye anajishughulisha na kazi ya fundi makenika, alitangazwa leo Jumatatu Mei 16, 2022 kuwa mshindi wa Jackpoti hiyo na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas.
“Ni furaha yangu kubwa sana kwa niaba ya kampuni kumtangaza kwenu Florian Valerian Massawe kuwa ni mshindi rasmi wa Jackpot yetu akiwa amejishindia Sh1.2 bilioni.
Tarimba aliongeza kuwa tayari kampuni hiyo imeshakamilisha malipo ya kiasi hicho cha fedha kwa mshindi.
“Hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni ya kubashiri kumtangaza mshindi wa kiasi kikubwa (Bilioni 1.2) kwenye sekta ya michezo ya kubashiri na kwenda kukabidhiwa pesa yake.”
“Fedha hizi alizoshinda tayari zipo kwenye akaunti yake ya SportPesa na tunafuata utaratibu ili kuhakikisha tunamkabidhi maana malipo yetu sisi ni papo hapo mara baada ya kuibuka mshindi,“ amesema Tarimba
Ni miaka mitano sasa tangu kuanzishwa kwa kampuni ya Sportpesa ikiwa imetangaza jumla ya washindi nane wa Jackpot.
Hongera kwake
ReplyDelete